Rozari takatifu ni sala kutoka Mbinguni. Bikira Maria alimkabidhi Mtakatifu Dominiki mwaka 1214 katika msitu wa Toulouse ambapo alienda kwa mafungo. Huko alisali usiku na mchana bila kula wala kunywa akifanya toba na malipizi.
Usiku wa siku ya tatu alizimia ndipo Bikira Maria alimtokea akiwa amefuatana na malaika watatu na alimkabidhi Mtakatifu Dominiki Rozari Takatifu, kisha akamfundisha namna ya kuisali. Alimfundisha matendo ya furaha, uchungu na utukufu kwa maana ya kusali tasbihi tatu ambazo ni Rozari moja. Papa Yohane Paulo wa II mwaka 2002 aliongeza matendo ya mwanga ambapo sasa tunasali tasbihi nne ambazo ni Rozari moja.
Malengo ya Rozari Hai ni kama yafuatayo: