• Mwanachama anapaswa kusali kila siku kumi lake na kutafakari wakati huo fumbo la Rozari linalohusika na kumi hilo. Bila ushirikiano wako. Rozari Haiwezi kuwa hai na hivyo kupoteza thamani yake.
  • Kila mwanachama anashauriwa kufanya saa takatifu mbele ya Yesu. Ekaristi kwa muda wa nusu saa, na/au afanye njia ya msalaba kwa kuwaombea wanachama wa Rozari waliofariki.
  • Kila mwezi Mei kila mwanachama ajitahidi kumheshimu Bikira Maria kwa kufanya ibada zake. Ni vizuri kila mwanachama asali Rozari nzima kila jumapili ya kwanza ya mwezi wa kumi (Oktoba) , ambayo ni sikukuu ya  ROZARI TAKATIFU.
  • Kila mwanachama ajitahidi kuwasaidia wagonjwa na kuona kuwa wanapata sakramenti, pia awashauri na kuwasaidia katika mahitaji yao ya kawaida.
  • Kila mwanachama ajitahidi kuwaombea wagonjwa na wale wanaofariki.
  • Wanachama wasisahau nia ya ibada hii takatifu kama ilivyoelezwa na Papa Gregori XVI mnamo Januari 27,1832 akisema: “ Tunajilazimisha kuwasha mioyo ya waumini wote wapate; Juhudi, Heshima, Upendo na Ibada kwa Mama yetu mtakatifu. Tunajibidisha kuongeza bidii ili kila mmoja wetu aweze kuendeleza zoezi hili, ili idadi ya wanachama na rehema zipatikanazo, ziongezeke sana. Tunajitahidi sana kuwa wapenzi wa Mama Mtakatifu wa Mungu, ambaye anaahidi kuwaongoza mbinguni wote wanaomheshimu kwa ibada hii. Tutafurahi sana iwapo tutakuwa tumefungua chemchemi kubwa ya Baraka za Mungu na afya kwa waumini wote kwa njia ya ibada hii ya Rozari Hai.”