Bikira Maria aliwatokea watoto watatu Lusia, Francisco na Yasinta huko Fatima Ureno kwa mara ya kwanza tarehe 13/05/1971 na aliendelea kutokea mara sita hadi tarehe 13/10/1917 alipotokea kwa mara ya mwisho. 

TOKEO LA KWANZA 13/05/1917: 
UJUMBE: 
Kujitoa kwa ajili ya Mungu 
Kupokea mateso kwa ajili ya malipizi ya dhambi nyingi za kumkosea Mungu na utukufu wake. 
Kuomba kwa ajili ya wongofu wa wakosefu
Salini Rozari kila siku ili kupata amani Duniani. 

TOKEO LA PILI 13/06/1917: 
UJUMBE: 
Yesu anataka kuanzisha ibada kwa Moyo wangu safi, ninaahidi kwamba watu watakaonifuata wataongoka. Roho zile zitampendeza Mungu sana kama maua ninayopeleka kwenye kiti chake cha enzi. Msikate tama sitawaacha ninyi. Moyo wangu safi utakuwa tegemeo leni katika mateso yenu ya mbele ya njia itakayowaongoza ninyi kwa Mungu. 
Salimi Rozari kila siku.

TOKEO LA TATU 13/07/1917: 
UJUMBE: 
Kufanya majitoleo kwa ajili ya wakosefu
Aliwaonyesha Lusia, Franciska na Yasinta motoni ambako wakosefu huenda 
“Adhabu ya dunia inakaribia kwa sababu ya dhambi nyingi, vita, njaa, na madhulumu ya Kanisa. 
“Kwa ajili ya kuzuia hayo nitaomba kuukabidhi moyo wangu safi nchi zile zote zinazomkana Mungu”. 
“Mungu anataka kuanzisha duniani ibada kwa moyo wangu safi, mkifanya ninayowaambia Roho nyingi zitaokolewa na itakuwepo amani Duniani”. 
“Komunyo Takatifu ipokelewe kwa malipizi ya dhambi kila jumamosi ya kwanza ya mwezi”. 
“Mnaposali Rozari semeni mwishoni utukinge na moto wa milele, uongoze roho zote mbingu hasa za wale wanaohitaji zaidi huruma yako”. 

TOKEO LA NNE 19/08/1917: 
UJUMBE: 
“Salini, salini mkatolee sadaka nyingi kwa ajili ya wakosefu kwa sababu wengi wanakwenda motoni kwa kuwa hayuko mtu anayewaombea wala kujitolea sadaka kwa ajili yao”. “Salini kila siku”. 
    

TOKEO LA TANO 13/09/1917
UJUMBE: 
“Endeleeni kusali Rozari ili vita iishe. Nitarudi mwezi Oktoba pamoja na Mt.Yoseph na Mtoto Yesu”. “Mwezi ujao Oktoba nitafanya muujiza ili watu wote wasadiki”. 
TOKEO LA SITA 13/10/1917: 
UJUMBE: 
Mimi ni Malkia wa Rozari na kwamba kikanisa kijengwe kwa heshima yangu mahali hapa. 
Watu waendelee kusali Rozari kila siku, vita vitaisha na wanajeshi watarejea nyumbani. 
Watu watubu na kuomba misamaha ya dhambi zao
Watu wasimkosee tena Mungu kwa maana wamemkosea mara nyingi mno mpaka sasa. 
Kwa ujumla katika matokeo ya Fatima Mama Bikira Maria alisisitiza watu waache dhambi, wafanye toba, wamrudie Mungu na wasali Rozari kila siku. 
(Waimbe wimbo: ,,Sisi wana wa dunia, tukumbuke maneno aliyosema…..)