Rozari hai ni njia ya kusali Rozari (tasbihi4) kwa njia ya kusali watu 20. Watu hawa 20 hushirikiana kusali Rozari nzima kwa jinsi kila mmoja wa watu hawa 20 anasali kumi na moja tu na kutafakari fumbo linalohusika na kumi hilo. 

Kumi linajumuisha “Fumbo husika, Baba yey x1, Salamu Maria x10 zikiambatana na tafakari za fumbo husika, Atukuzwe Baba x1 na Ee Yesu mwema…….”

Hivyo watu watano wa kwanza wanagawana mafumbo matano ya furaha, watano wanaofuata mafumbo matano ya mwanga, watano wengine wanagawana mafumbo matano ya uchungu na watano waliobakia wanagawana mafumbo ya utukufu. 

Kila mmoja wa watu hawa ishirini akisali kumi lake moja alilogawiwa na makao makuu anapata neema na mastahili ya Rozari nzima (tasbihi 4) yaani mafumbo yote ishirini. Kila mwanachama aliyejiunga na Rozari Hai atatakiwa awe mwaminifu kusali kumi lake kila siku kwa maisha yake yote. Vinginevyo Rozari hiyo haiwezi kuwa Hai tena. 

Rozari haina na Rozari takatifu ni kitu kile kile isipokwa Rozari hai ni njia tu ya kusali Rozari takatifu kwa kushirikiana na watu ambao hawakai pamoja na kwa muda tofauti. 

Wanachama wa Rozari Hai hawahitaji kukusanyika ili kusali makumi yao, ila kila mmoja anasali kumi lake mahali popote, wakati wowote, mara moja kila siku. Kwa wale walioamua kusali Rozari nzima kila siku yaani tasbihi nne, mafumbo ya furaha, mwanga, uchungu na utukufu hawana tena ulazima wa kusali kumi lingine kutimiza Rozari yao hai. Wanachotakiwa kufanya ni kuweka nia wanaposali kumi lao lakini haikatazwi kuongeza kumi jingine ni hiyari yako. Nia ya Rozari Hai ni kwa ajili ya USHINDI  WA MOYO IMAKULATA WA MARIA NA KWA HESHIMA YA MTAKATIFU FILOMENA MSIMAMIZI WA ROZARI HAI ULIMWENGUNI.
Wanachama wanaoandikishwa ni watu wazima, vijana na watoto wanaofahamu sala. Watoto hawa waandikishwe chini ya uangalizi wa wazazi wao au walezi wao. Wanachama wote huandikishwa rasmi na kupewa kadi maalum inayoonyesha siku ya kuanza kusali. Kwa wale wanachama ambao waliandikishwa zamani hawana haja ya kujiandikisha tena kama walipoteza kadi watoe taarifa ili wapewe kadi zingine zenye taarifa zilezile na kumi lake lilelile kwani kumbukumbu za wanachama wa zamani zimehifadhiwa.
Mtu wa anayesali tendo la kwanza ndiye anaanza na sala ya Nasadiki, Baba Yetu…, Salamu Maria tatu…., Atukuzwe Baba….. , Sala ya Utangulizi, Sala kabla ya Tafakari, Nia ya Rozari Hai, Baba Yetu, Salamu Maria x10 kwa kutafakari fumbo hilo(tafakari kabla ya kila Salamu Maria), Atukuzwe Baba…  na Ee Yesu wangu.
Mtu wa tendo la pili hasali sala ya Nasadiki. Anaanza na sala ya Utangulizi, Sala kabla ya Tafakari Nia ya Rozari Hai, Baba Yetu, Salamu Maria x10 kwa kutafakari fumbo hilo(tafakari kabla ya kila Salamu Maria), Atukuzwe Baba…  na Ee Yesu wangu.
Kadhalika mtu wa Tendo la la tatu na nne pia atasali kwa utaratibu huo wa mtu wa tendo la pili.
Mtu wa Tendo la tano hasali sala ya Nasadiki. Anaanza na sala ya Utangulizi, Sala kabla ya Tafakari Nia ya Rozari Hai, Baba Yetu, Salamu Maria x10 kwa kutafakari fumbo hilo(tafakari kabla ya kila Salamu Maria), Atukuzwe Baba…  Ee Yesu wangu na atamalizia na sala ya Salamu Malkia na Kumbuka.