Malengo ya Rozari Hai ni kama yafuatayo:

  • Kutuliza hasira ya Mungu aliyekasirishwa na dhambi zetu nyingi mno.
  • Tunamtuliza kwa njia ya maombi ya Mama Maria.
  • Kulinda na kufufua Imani katika roho za Wakristo, na kuwaongoa wakosefu.
  • Kadhalika tunaongeza utukufu wa Mama Kanisa.
  • Kuleta ushindi wa Moyo safi wa Maria. Ushindi ambao aliutabiri Maria katika matukio ya Fatima: “Moyo wangu safi mwishowe utashinda!”
  • Kwa kumheshimu Mt.Filomena aliye somo na mlinzi wa Rozari Hai.
  • Kwa kuwaombea Maaskofu, Mapadri, Watawa, Wagonjwa na Wanaokufa leo ili wapate kifo chema. Kadhalika kwa kuomba Amani katika familia zetu.
  • Kumfanya shetani asiweze tena kuwa na nguvu saa ya kufa kwetu.