*Sababu nzuri za Kusali Rozari*
1.Kupata amani duniani _(Bibi Yetu wa Fatima, 1917)_

2.Kulinda amani katika familia _(Papa Pio XII)_

3.Kuwa na ujasiri katika Changamoto za maisha ya kila siku_(Papa Leo wa XIII)_

4.Njia iliyo tayari na rahisi kulinda imani _(Papa Leo XIII)_

5.Kutia moyo wakati wa maisha ya shida _(Padre Peyton)_

6.Kupata ulinzi wa mwisho _(Askofu Hugh Boyle)_

7.Njia iliyotayari na Rahisi ya kuilinda Imani _(Papa Leo XIII)_

8.Inaponya maovu Yetu ya Kila Siku _(Papa Pio XII)_

9.Ni njia ya kuufikia Ukamilifu wa Kristo _(Papa Yohane XXIII)_

10.Kwa ajili ya Mafanikio katika maisha  ya Wito ulioitiwa. _(Marshal Foch, Jemadari Mkuu katika Vitaya Kwanza yaDunia)_

11.Ni njia ya kujipatia Neema kutoka kwa Mungu _( Papa Pio IX)_

12.Kwa ajili ya kudumu mpaka siku ya Mwisho. _(Askofu Hugh Boyle)_

13. Kwa ajili ya Utii kwa Mama wa Mungu Malkia wa Rozari Takatifu. _-(Papa Yohane Paulo II)_

*AHADI ZA BIKIRA MARIA KWA SALA YA ROZARI:*
1.Ninawaahidi wote watakaosali Rozari yangu kwa ibada ulinzi wangu wa pekee na neema kubwa.

2.Ninaahidi kinga zangu maalum na Baraka nyingi kwa wote

 3.watakaosali Rozari.
Rozari itakuwa kinga madhubuti dhidi ya Motoni,  itaangamiza maovu, kupunguza dhambi na kuushinda upotoshaji.

4.Itawezesha karama na kazi nzuri kudumu, itapatia nyoyo huruma nyingi za Mungu. itaondoa kutoka mioyo ya wanadamu tamaa za kidunia na madhara yake na kuziinua ziitamani mbingu. Ingefaa sana nyoyo zingejitakasa kwa njia hii.

5.Nyoyo zitakazojipendekeza zenyewe kwangu kwa sala ya Rozari takatifu hazitaangamia.

6.Yeyote atakayesali Rozari *kwa unyenyekevu, akitafakari na kuishi mafumbo matakatifu hatapatwa na majanga. Mungu hatamuadhibu wakati wa hukumu yake, hatakufa kifo kisichopangwa,* akiwa ni mtu wa haki atabaki katika Baraka za Mungu na kupata mastahili ya mbinguni.

7.Yeyote atakayekuwa na mapendo halisi ya Rozari Takatifu hatakufa bila sakramenti za Kanisa.***

8.Wale watakaokuwa waaminifu kwa sala ya Rozari Takatifu watapata mwanga wa Mungu na Baraka maridhawa, wakati wa maisha na kifo chao, watashiriki katika mastahili ya watakatifu mbinguni wakati wa kufa.

*9*Nitawatoa toharani* *wote watakaodumu katika kusali Rozari*

10.Watoto waaminifu wa Rozari watazawadiwa utukufu mkubwa mbinguni.

11.Utapata yote utakayoomba kwa sala ya Rozari.

12. *Wote watakaoeneza ibada ya Rozari Takatifu nitawazawadia katika mahitaji yao mema katika shida zao zote.*

13.Nalipata kwa mwanangu neema kwa ajili ya wanachama wa Rozari, nayo ni hii *“wanachama watawapata watakatifu wa mbinguni kama ndugu zao wapate kuwasaidia katika maisha na saa ya kufa”.*
 
14. *Wote wanaosali Rozari yangu kikamilifu ni watoto wangu wapendwa, ni kaka na dada wa Yesu Kristo mwanangu.

15.Upendo wa Rozari ni ishara kubwa ya uongofu wa milele. *Walio na Ibada kuu kwa Rozari yangu hawatakufa bila kutulizwa na Mama Kanisa katika Sakramenti.*