Ee Bwana, utujalie tunakuomba, wakati tunapotafakari mafumbo ya Rozari ya Mama Maria, tuige yale tunayotafakari ili tupate yale tunayoahidiwa. Kwa Kristu Bwana wetu. Amina.

Na sasa tuungane na wanachama wa jumuiya ya Rozari Hai duniani kote na kutolea fungu hili la Rozari Takatifu kwa: Ushindi wa Moyo Imaakulata wa Maria, kwa heshima ya Mt. Filomena, Mwenyeheri Paulina Marie Jaricot na Mt. Theresia wa Mtoto Yesu; kwa ajili ya nia za Baba Mtakatifu, kwa ajili ya maaskofu wote, kwa ajili ya Mapadre, na watawa wanachama, wagonjwa na wanaoteseka; na watakaokufa leo ili wapewe neema za uvumilivu na hatimaye kifo chema, pia kwa ajili ya amani katika familia zetu.
          …….Fungu langu ni……


SALA BAADA YA TAKAFAKARI
Ee Maria, uliyeumbwa pasipo dhambi ya asili, tunaomba kupitia kwako upendo mtilifu kwa Mwanao Yesu Kristu!
Ee Roho Mtakatifu, tunakutolea Moyo wa Kiekaristi wa Yesu, Damu yake Takatifu; Moyo Imakulata wa Maria wenye uchungu, mpole, mnyenyekevu na mtiifu, kwa ajili ya kulipia dhambi zetu pamoja na madharau yetu. Tunajitolea kwako kabisa. Tunaweka nafsi zetu mikononi mwako.Amina