Tafakari ya mafumbo ya Rozari ni sehemu iliyo muhimu sana katika Sala ya Rozari. Tukiacha tafakari. Rozari yetu itabaki kama vile mwili bila roho. Mama  Maria alipomfundisha Mt. Dominiki namna ya kusali Rozari. Alimsisitiza sana kufanya tafakari ya mafumbo ya Rozari. Bikira Maria alimwambia: “Watu wanaposali Salamu Maria mara mia moja na hamsini (Rozari nzima) wananipendeza sana. 

Lakini nitafurahi zaidI iwapo watasali salamu Maria hizo huku wakitafakari maisha, mateso, kifo na ufufuko wa Yesu, ambavyo vimo kwenye mafumbo.” Hivyo tafakari ndio roho ya Rozari. Hivyo  tafakari ni jambo muhimu sana katika ibada ya Rozari takatifu.

Kuna njia kadhaa za kufanya tafakari ya mafumbo ya Rozari. Hapa nimependekeza njia mojawapo ninayoiona itatufaa wote. Njia niliyochagua ni ile ya kugawa kila fumbo katika mawazo kumi kulingana na salamu Maria kumi. Kabla ya kila salamu Maria  ya kumi lake, unataja wazo moja na  kulitafakari wakari unaposali Salamu Maria hiyo. Hivyo kwa kila salamu Maria unataja wazo moja na kulitafakari. Kwa njia hii utakuwa umefanya tafakari nzuri sana. Tafakari hizi zinapatikana katika vitabu vya Kanuni ya Rozari Hai.

“ uwezo wa Mungu Ni Mikononi Mwako
Sali Rozari yako kila siku!